BOOMPLAY INASHEHEREKEA WANAMUZIKI WA KIKE KATIKA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

0
Booom Play App

Boomplay ni app nambari moja kwa huduma ya kusikiliza na kupakua
muziki barani Afrika, inasherehekea Siku Ya Wanawake Duniani 2019 ikiwa
na kampeni mpya ya “Boom Queens”.


Vanessa Mdee, Rihanna, Tiwa Savage, Fena Gitu na wengine wengi, ni
miongoni mwa  wanawake wenye vipaji ambao wameendelea kubadilisha tasnia
ya muziki duniani. App ya Boomplay itakuwa na muonekano wa tofauti hasa
katika Siku Ya Wanawake duniani tarehe 8 Machi, lengo likiwa ni
kuonesha na kukuza kazi za wanawake katika muziki. App itapambwa na
nyimbo, albamu pamoja na playlist za wanawake katika vipengele vyote
kwenye ukurasa wa kwanza.


Boomplay pia itakuwa na kampeni kabambe ambayo itatoa fursa ya kukuza
mauzo ya kazi za wanawake ambao nyimbo zao zitakuwepo kwenye playlist
ya BOOM QUEENS. Playlist hiyo itakuwa na nyimbo za wasanii bora wa kike
tu.


Katika kampeni hii, Meneja Mahusiano wa kampuni ya Boomplay, Bi Tosin
Sorinola amesema, “majadiliano juu ya usawa wa kijinsia ni moja ya
mambo ambayo ni muhimu kwetu kama jukwaa lenye nia kubwa ya kukuza
wanawake katika muziki, katika njia njema kadri iwezekanavyo. Kampeni
hii sio kwa mara moja tu, ni endelevu, na hili litadhihirishwa katika
shughuli zetu za kila siku”.


Katika mwezi huu wa kuadhimisha Siku Ya Wanawake Duniani, watumiaji
wa Boomplay kupitia simu zao za Android na iOS watapata fursa ya
kujishindia simu mpya ya iPhone XS na zawadi nyingine kem kem nchini
Tanzania, Kenya, Nigeria na Ghana. Ili kuonesha upendo kwa wasanii wa
kike katika tasnia ya muziki, basi jishindie zawadi hizi kwa
ku-subscribe kwenye app ya Boomplay kwenye vifurushi vinavyopatikana
(vya siku, wiki na mwezi) na pia sikiliza playlist ya Boom Queens.


App ya Boomplay ambayo ina watumiaji zaidi ya milioni 42 dunia kote,
hivi karibuni ilizindua app hiyo kwenye jukwaa la iOS. Hakika Boomplay
inajivunia kuwa na nyimbo na video zaidi ya milioni 5 kutoka kwa wasanii
wa Tanzania na wakimataifa.