Boomplay kuboresha tasnia ya muziki nchini Tanzania, yatangaza kushirikiana zaidi na wasanii wa Tanzania

0

Dar es Salaam Boomplay, app inayoongoza barani Afrika kwa huduma ya
kusikiliza na kupakua muziki, yafanya forum yake ya kwanza kwa ajili ya
wasanii nchini Tanzania.
Katika forum hiyo, Meneja wa Boomplay Tanzania Bi Natasha Stambuli
alizungumza kuhusu kuwezesha wasanii na uzalishaji wa muziki
(Production) na usambazaji wa muziki kidigitali (Digital Distribution).
 
“Boomplay tunatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili wasanii
kama kupata muda wa studio, ku-shoot video zenye quality ya kimataifa na
mengine mengi. Tumeingia mkataba na Wanene Entertainment ili kuwezesha
wasanii na matatizo hayo.”
“Barani Afrika Boomplay ina ofisi Tanzania pamoja na Kenya, Nigeria
na Ghana. Moja kati ya fursa zinazopatikana ni sisi kuwa na uwezo wa
kujenga madaraja kwa wasanii wetu wa Tanzania na wasanii wengine kutoka
nchi hizo” aliendelea Bi Natasha Stambuli.
Forum hiyo ilijumuisha jopo la wataalamu mbalimbali katika tasnia ya
muziki akiwemo Bi Martha Huro – Meneja wa Boomplay Kenya, Lupakisyo
Mwambinga – Mkuu wa Idara Ya Sheria COSOTA, Nahreel kutoka Navy Kenzo,
Moses Range – Muanzilishi DEMO Innovators, Japhet Kapinga – Meneja
Maudhui Boomplay na kuratibiwa na msanii wa miondoko ya Hip Hop, Wakazi.
Wasanii na watayarishaji pia walipata nafasi ya kuuliza maswali kwa
wataalamu hao na kupata ujuzi zaidi katika masuala ya sheria, hati
miliki, branding na vingine vingi katika tasnia ya muziki.
Kuhusu Boomplay
Boomplay (ambayo awali ilikuwa ikifahamika kama Boomplayer), ni
jukwaa linalotoa huduma ya kusikiliza na kupakua (download) muziki
ambayo ipo chini ya umiliki wa kampuni ya Transsnet Music Limited.
Malengo ya app hii ni kutengeneza jukwaa kubwa na la kutegemewa na
wasanii na wazalishaji wa muziki katika usambazaji wa kazi hizo za
sanaa. Kwa sasa Boomplay ndio application kubwa na inayokuwa kwa kasi
sana barani Afrika, ikiwa na nyimbo na video zaidi ya milioni 5.
Watumiaji wake wanaweza kusikiliza na kuangalia video bure, kwa
kujisajili (subscribe) kupitia vifurushi vya siku,wiki au vile vya mwezi
ambapo ambavyo vinawawezesha kuhifadhi (save) nyimbo offline au kununua
nyimbo. Huduma hiyo kwa sasa inapatikana Android, iOS na wavuti.

LEAVE A REPLAY / COMMENT: